Rais Dkt. Samia atoa msamaha kwa Wafungwa 4,877

Katika kuadhikisha Miaka 61 ya Muungano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametumia mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1) (a) – (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa msamaha kwa wafungwa wa makundi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wafungwa elfu nne mia nane themanini na saba (4,887) wamenufaika na msamaha huu ambapo arobaini na mbili (42) kati yao wanaachiliwa huru tarehe 26 Aprili, 2025 na elfu nne mia nane arobaini na tano (4,845) wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.

“Ni matarajio ya Serikali kuwa  wafungwa  hao  watarejea  tena  katika  jamii  kushirikiana  nawananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.” – Imeeleza Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani.