Rapa Latto Athibitisha Kuwa Penzini Na Rapa 21 Savage.

Rapa Wa Marekani Big @latto amethibitisha Rasmi kwamba yeye na Rapa @21savage wako kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Ripota Wa TMZ Alikutana na rapa huyo mitaa ya New York Na kumuuliza kama amechoka kuulizwa kuhusu “mtu fulani.” Alipoulizwa zaidi, ikabainika mtu huyo ni Rapa 21 Savage. Ambapo Latto Alijibu Akisema….. hajachoka, Huku Akisisitiza kwa furaha: “My man, my man, my man, my man”

Kumbuka Kuwa tetesi za uhusiano wao zimekuwa zikisambaa tangu Desemba 2020, Ambapo Wamekuwa wakilifanya Penzi Lao kuwa siri (privately) Kwa muda mrefu.