Rapa Tyga Kwenye Penzi Jipya Na Muigizaji ‘Madelaine’

Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali, Rapa Tyga Na Muigizaji Mrembo “Madelaine Petsch” Sasa Rami Ni Wapenzi. Vyanzo Vya Karibu Vimeiambia TMZ Kuwa Rapa Huyo Na Muigizaji Wa Filamu Ya “Riverdale” (Madelaine) Wameanza Mahusiano Yao Ya Kimahaba Hivi Karibuni.

Tarehe 19 Februari 2025, Tyga na Madelaine walionekana pamoja wakihudhuria mchezo wa mpira wa kikapu kati ya Los Angeles Lakers na Charlotte Hornets katika ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles. Madelaine alivaa koti jeusi la ngozi na suruali ya jeans, huku Tyga akiwa amevalia koti la njano la “letterman.” 

Siku chache baadaye, tarehe 26 Februari 2025, walihudhuria pamoja tafrija ya Vanity Fair na Instagram’s Vanities Party. Katika tukio hilo, Madelaine alivaa gauni jeusi la velvet lenye uwazi, na Tyga alivaa mavazi ya ngozi meusi. Ingawa walionekana wakiingia pamoja huku wakiwa wameunganisha mikono, walitembea kwenye zulia jekundu kila mmoja kivyake. 

Vyanzo vya karibu vimeeleza kuwa Tyga na Madelaine wamekuwa wakifurahia muda pamoja na kwamba uhusiano wao umeanza hivi karibuni. Hata hivyo, wawakilishi wa wawili hao hawajatoa maoni yoyote kuhusu uvumi huu. 

Kabla ya uhusiano huu, Tyga alikuwa kwenye mahusiano na Avril Lavigne, Chanel Iman, Kylie Jenner, na Blac Chyna, ambaye wana mtoto pamoja. Madelaine, kwa upande wake, alihusishwa na Anthony Li, na kabla ya hapo, alikuwa kwenye uhusiano na Travis Mills. 

Ingawa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Tyga na Madelaine kuhusu uhusiano wao, mashabiki na vyombo vya habari vinaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wawili hawa maarufu.