Rashford kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Barcelona

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford, sasa anapatikana sokoni kwa vilabu vyote kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 40.

Taarifa zinaeleza kuwa Rashford bado yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na klabu ya Barcelona, tangu mwezi Januari mwaka huu.

Hata hivyo, dili hilo halikufanikiwa wakati huo kwa sababu hakukuwa na mchezaji yeyote aliyeuzwa ili kufanikisha uhamisho huo.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa mwandishi Toni Juanmartí (@tjuanmarti), wawakilishi wa Rashford wamekutana tena na viongozi wa Barcelona, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mazungumzo.

Rashford anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wanne waliopo kwenye orodha ya Barcelona, wanaotazamwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao msimu ujao.

Mpaka sasa, haijathibitishwa rasmi iwapo mazungumzo hayo yameleta mafanikio, lakini uwezekano wa Rashford kujiunga na Barcelona bado uko wazi.