Ratcliffe akanusha United kuuza wachezaji kujikwamua na ukwasi

Mmoja wa wamiliki wenza wa klabu ya Manchester United bwana, Jim Ratcliffe amekataa tetesi za kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji wake ili kupata faida na kujikwamua kiuchumi.

“Tuwauze Mainoo na Garnacho ili tupate faida? Hapana, hapana. Hatutauza wachezaji kwa sababu ya hali yetu ya kifedha”

“Klabu ilikuwa imejaa sana, kwa hivyo tumepunguza hilo na tutamalizia kwa kuwa na taasisi inayojitosheleza na yenye ufanisi, hivi ndivyo tutakavyoshughulikia gharama,” amesema Ratcliffe.