Ratcliffe athibitisha Sancho kurudi Man United

Mmoja wa wamiliki wenza wa klabu ya Manchester United bwana, Jim Ratcliffe ameweka wazi suala zima la Jadon Sancho kurejea katika kikosi cha Manchester United.

“Kuhusu Sancho,ambaye kwa sasa anachezea Chelsea na tunalipa nusu ya posho yake, tunalipa pauni £17m zaidi ya Tsh. bilioni 57.

Ratcliffe aliwahi kuhojiwa na aliwataja wachezaji kama Casemiro, Antony, Jadon Sancho, Rasmus Højlund, na André Onana kuwa “hawatoshi” na “wanalipwa kupita kiasi.”

Alisisitiza kuwa matatizo hayo yanatokana na maamuzi yaliyofanywa kabla ya umiliki wake na kwamba itachukua muda kubadilisha kikosi.

Aidha ameongeza kuwa United italipa pauni £89m zaidi ya Tsh bilioni 300 katika majira ya kiangazi kwa wachezaji ambao hawajasajiliwa na hata kama itatokea hawatawasaliji wachezaji hao bado wanalazimika kuandika hundi ya pauni £89m kuwalipa wachezaji hao.