Mkurugenzi Mtendaji wa Real Betis, Ramón Alarcón ameweka wazi mipango ya klabu hio kuhitaji Saini ya, Anthony ambaye yupo klabuni hapo kwa mkopo akitokea Manchester United.
Ramón amezungumza hayo baada ya kuulizwa na waandishi kuhusu mustakabali wa Anthony kama atasalia klabuni hapo kwa misimu zaidi.
“Kwanini tusimuache hapa Anthony msimu ujao?? inawezekana, tumetuma taarifa zote kwa United hatua zote na maelezo ya mchezaji kwa wiki nzima ili waone kuwa tunamtunza mchezo wao”
“Kuna muunganiko mzuri sana kati yake na wachezaji wenzie,” amesema Alarcon.
Anthony amecheza michezo miwili mpaka sasa na amefanikiwa kuchukua mchezaji Bora wa mechi mara zote mbili akitoa pasi ya goli katika mechi ya kwanza na kufunga goli katika mechi ya pili.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.