Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally leo Machi 26, 2025 amezindua kauli mbiu mpya kuelekea mchezo wao wa Robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo amesema kauli mbiu yao kwasasa ni ‘HII TUNAVUKA’.
“Kauli mbiu ya mchezo dhidi la Al Masry itakuwa ni HII TUNAVUKA. Hii inamaanisha kwamba kwa misimu mitano mfululizo tunaishia robo fainali lakini safari hii tunavuka kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu,” amesema Ahmed.
Simba wataikaribisha Al Masry kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Jumatano ya Aprili 2, 2025 kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza utakaoanza kutimua vumbi kuanza saa 1:00 usiku.
Mchezo wa marudiano umepangwa kufanyika tarehe 9 Aprili 2025, ambapo Simba SC watawakaribisha Al Masry.
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limemteua mwamuzi kutoka Mali, Boubou Traore, kuendesha mchezo huu wa kwanza wa robo fainali kati ya Al Masry na Simba SC.
Mshindi wa jumla kati ya Simba SC na Al Masry atakutana na mshindi kati ya Zamalek SC ya Misri na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.