Tanga wampa tano Rais Samia kwa utendaji kazi wake

Baadhi ya wananchi kutoka Mkoani Tanga wametoa maaoni yao baada ya kumalizika kwa siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambapo wamekiri utendaji kazi mahiri wa Rais Samia pamoja na chachu kubwa ya maendeleo ndani ya mkoa huo.

Baadhi ya wananchi hao wameonyesha kufurahishwa na Utendaji kazi wa Rais Samia kwa kuwa umegusa maeneo yote muhimu ikiwemo huduma ya Afya na Elimu. 

Aidha wamesema wana imani na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na zawadi pekee watakayompa ni kumchagua katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.