Tanzia: Spika Mstaafu Job Ndugai afariki Dunia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Spika Mstaafu na aliyekuwa Mbunge wa Kongwa Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, kilichotokea leo tarehe 06 Agosti, 2025 Jijini Dodoma.

“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasiasa mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea leo jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na Wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Mheshimiwa Spika.