Ten Hag atimuliwa Bayer Leverkusen

Kocha, Erik ten Hag ametimuliwa na klabu ya Bayer Leverkusen, uamuzi uliothibitishwa rasmi leo baada ya ripoti zilizokuwa zikisambaa mapema kuhusu mustakabali wa kocha huyo.

Ten Hag, ambaye alijiunga na Leverkusen akitarajiwa kuendeleza mafanikio ya klabu hiyo, hakuweza kuonyesha matokeo yaliyotarajiwa na uongozi. Ripoti zinaeleza kuwa mwenendo wa timu pamoja na presha kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka ulisababisha bodi kufanya maamuzi ya haraka.

Bayer Leverkusen sasa wako katika mchakato wa kumtafuta mrithi wake, huku majina kadhaa ya makocha wenye uzoefu yakihusishwa kuchukua nafasi hiyo.