The Weeknd Anunua Jumba La Kifahari Kwa Tsh. Bilioni. 135/=.

The Weeknd sio wa mchezo! anaumaliza mwaka kwa kuonesha jeuri ya fedha, Kwani Amenunua Jumba La Kifahari Yenye thamani ya dola milioni 55 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 135/=.

Jumba hilo la kifahari lipo Karibu Na Fukwe huko Miami, Florida Nchini Marekani, lina vyumba 8 vya kulala, mabafu 10, bwawa la kuogelea (Swimming Pool), sehemu ya mazoezi, studio ya muziki na mengine mengi.

Mwaka 2021 The Weeknd Pia Alinunua Mjengo Wa Maana kwenye eneo waishio watu maarufu Bel-Air mjini Los Angeles, California. Kwa mujibu wa The Wall Street Journal, The Weeknd alinunua mjengo huo kwa ($70 million) sawa na TSh. BILIONI 171.8/=.