Kwa mara ya kwanza katika historia, TikTok imepigwa marufuku rasmi nchini Marekani, hatua ambayo imewafanya mamilioni ya watumiaji wake kushindwa kufikia programu hiyo pamoja na huduma zake zote. Hatua hii imeibua mijadala mikubwa mitandaoni, huku wengi wakielezea maoni yao kuhusu athari za marufuku hiyo kwa wabunifu wa maudhui na biashara zinazotegemea jukwaa hilo.
Marufuku hiyo inatajwa kuwa ni sehemu ya juhudi za serikali ya Marekani kudhibiti usalama wa data na kuzuia kile kinachoelezwa kuwa ni tishio kutoka kwa programu zinazomilikiwa na kampuni za kigeni, hususan China.

Hata hivyo, baadhi ya watumiaji wamesikitishwa na hatua hiyo, wakisema TikTok ilikuwa chanzo kikubwa cha burudani, ajira, na mawasiliano kwa watu wa rika zote. Wengine wanaona marufuku hiyo kama changamoto mpya ya kutafuta njia mbadala za kushirikiana mtandaoni.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.