Tiktok yatangaza kusitisha huduma zake Marekani Januari 19

TikTok imetangaza kuwa itasitisha shughuli zake nchini Marekani ifikapo Januari 19, 2025, endapo Mahakama Kuu haitasitisha au kuchelewesha agizo linalotaka ByteDance kuachia umiliki wa kampuni hiyo.

Sheria iliyopitishwa mwezi Aprili 2024 inalenga masuala ya usalama wa taifa, huku Mahakama Kuu ikitarajiwa kuamua kama wasiwasi huo unazidi haki ya uhuru wa kujieleza.

TikTok imethibitisha kuwa itafunga shughuli zake nchini Marekani kama sheria hiyo haitabatilishwa au kucheleweshwa, na kwa sasa, kampuni hiyo haipangi kuuza biashara yake kwenye soko la Marekani.