Rapa maarufu wa Marekani, Travis Scott, ameandika historia katika muziki wa kimataifa baada ya kujaza uwanja wa FNB Stadium uliopo jijini Johannesburg, Afrika Kusini, katika ziara yake ya dunia ya “Circus Maximus Tour.”

Tamasha hilo limevutia maelfu ya mashabiki, ambapo uwanja huo unaojulikana kuwa mkubwa zaidi barani Afrika mashabiki zaidi ya watu elfu 94 waliokuja kushuhudia show ya rapa huyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka Marekani kujaza FNB Stadium kwa kiwango hicho, jambo lililowafanya mashabiki na wadau wa muziki kusifia nguvu ya Travis Scott katika jukwaa la kimataifa.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.