Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza ushuru mkubwa kwa bidhaa kutoka mataifa mbalimbali katika kile alichokiita “siku ya ukombozi”, hatua inayozua wasiwasi wa kuzuka kwa vita vipya vya kibiashara duniani.
Kulingana na tangazo hilo, nchi za Umoja wa Ulaya sasa zitakabiliwa na ushuru wa asilimia 20 kwa bidhaa zinazoingia Marekani, China ikitozwa asilimia 34 huku nchi ya kusini mwa Afrika ya Lesotho ikiwekewa kiwango cha ushuru wa asilimia 50.
Mataifa kadhaa, yakiwemo Uingereza, Brazil, Mexico, Australia, Uswisi, na Poland, yamekosoa hatua hiyo ya Trump, yakisema si ishara ya urafiki na kwamba yako tayari kujibu vikali.
Hata hivyo, utawala wa Trump umeweka wazi kuwa hautaitoza ushuru mpya Urusi, kwa kuwa biashara kati ya mataifa hayo mawili imepungua maradufu tangu Marekani ilipoanza kuiwekea vikwazo Moscow kufuatia uvamizi wake wa Ukraine.
Hatua hii ni sehemu ya mpango wa “ushuru wa malipizano” ambao Trump aliwaagiza maafisa wake kuandaa mapema mwaka huu, akitekeleza ahadi yake ya kampeni ya “jicho kwa jicho” katika masuala ya biashara ya kimataifa.
Trump atangaza ushuru mkubwa kwa mataifa mbalimbali duniani

Leave a Reply