Universal Music Group (UMG) imewasilisha ombi la kufutwa kwa kesi ya Drake dhidi yao kuhusu wimbo Not Like Us, ikidai kuwa rapper huyo alishiriki kwenye “rap battle” kwa hiari na baadaye kushindwa.
UMG imesema Drake mwenyewe alichochea ushindani huo kwa kumshinikiza Kendrick Lamar ajibu mapigo, hata akatoa wimbo wa pili (Taylor Made) ili kuendeleza vita hiyo ya muziki.
Awali, Drake aliifuta kesi aliyofungua dhidi ya UMG na Spotify kuhusu madai ya kudanganya hesabu za streams za wimbo wa Lamar, lakini baada ya Super Bowl 2025, mawakili wake waliifungua tena kesi wakidai kuwa UMG ilimruhusu Lamar kutumbuiza Not Like Us, jambo waliloliona kama mwendelezo wa kashfa dhidi ya Drake.
Hata hivyo, UMG inataka kesi hiyo itupiliwe mbali, ikisisitiza kuwa Drake alishiriki mzozo huo kwa hiari na sasa analalamika bila sababu ya msingi.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.