United kumwaga zaidi ya 100b kupata saini ya Dorgu 

Inaonekana Manchester United wanaendelea na juhudi zao za kumsajili Patrick Dorgu kutoka Lecce. 

Mazungumzo yanaweza kuwa katika hatua za mwisho, hasa ikiwa vipengele vya makubaliano vitafikiwa kwa mujibu wa bei iliyowekwa ya (€40 milioni), takribani bilioni 106.

Kwa kuwa Dorgu tayari amekubaliana na masharti binafsi na United, sasa inasubiriwa makubaliano rasmi kati ya vilabu viwili. Hii inaweza kuwa usajili muhimu kwa United, ikizingatiwa kuwa Dorgu ni mchezaji chipukizi mwenye kipaji kikubwa.