Walker mambo safi, kujiunga na AC Milan

AC Milan wameanza mikakati ya kukamilisha usajili wa Kyle Walker, huku vipimo vya afya na hatua rasmi zikitarajiwa kufanyika kati ya Jumanne au Jumatano.

Beki huyo wa Manchester City ana hamu ya kuhamia Serie A, huku klabu hizo zikiwa katika mazungumzo ya mwisho ili kufanikisha makubaliano ya mkopo.