Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Masira amesema wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 2025, ni wakati wa CCM kukamata Dola na anaamini watakamata Dola kwa sababu kura ndizo zitakazosababisha CCM ishike Dola.
Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa uliofanyika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, Wasira amesema kuwa CCM imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule, hospital, miundombinu na kumalizia miradi iliyoachwa na Hayati Dkt. John Magufuli.
“Oktoba 2025 kazi ya kukamata dola itakamilika kwa kura kutokana na CCM kutekelea miradi ya maendeleo kwa wananchi.
“Katiba ya CCM ibara ya 5 imesema kazi ya CCM ni kushinda Uchaguzi na kukamata dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Wasira.
Leave a Reply