Wivu chanzo cha ugomvi kati ya Neymar Jr, Mbappe wakiwa PSG

Neymar anamwambia Romário: “Messi aliposajiliwa PSG nadhani Mbappe alipata wivu kidogo.

“Nilikuwa na mambo yangu naye, tuligombana kidogo. Alikuwa mdogo ambaye mwanzoni alikuwa kama ufunguo, nilizoea kumwita ‘Golden Boy’, nilizungumza naye, nilicheza naye karibu, nikamwambia atakuwa mmoja wa wachezaji bora, nilikuwa na mazungumzo naye kila wakati.

“Leo alipofika, aliona wivu kidogo, hakutaka kugawana upendo wangu kwake na mtu yeyote hapo ndipo ugomvi kati yangu mimi na yeye ulipoanza kukawa na mabadiliko ya tabia,” ameeleza Neymar Jr.