Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameunga mkono uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kutoa muda wa miezi mitatu kutoka sasa kuhakikisha Wawekezaji waliokodishiwa katika visiwa vidogo vidogo kuanza ujenzi mara moja katika visiwa hivyo na wakishindwa basi vitarudishwa serikalini
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Januari 7, 2025 wakati wa uzinduzi wa Hoteli ya Kifahari katika kisiwa cha Bawe kilichokodishwa kwa Mwekezaji visiwani Zanzibar
Rais Samia amesema uamuzi uliotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ni maamuzi sahihi ambayo itawafanya wawekezaji kufanya uwekezaji kwa wakati katika visiwa vidogo vidogo kama ambavyo imekusudiwa
Uwekezaji wa Hotel katika kisiwa cha Bawe umegharimu dola za Marekani Milioni Arobaini na Mbili ambao utatoa fursa za ajira za zaidi ya mia nne
Leave a Reply