Wizkid na Jada P Wabarikiwa na Mtoto wa Tatu
Nyota maarufu wa muziki kutoka Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun, anayefahamika kwa jina la kisanii Wizkid, na mpenzi wake wa muda mrefu, Jada Pollock, wamebarikiwa kupata mtoto wao wa tatu. Tukio hili la furaha limeongeza idadi ya watoto wa msanii huyo na kufikia jumla ya watoto watano.
Wizkid, ambaye ametoa hits nyingi kama Essence, Ojuelegba, na Come Closer, ameendelea kuwa mmoja wa wasanii wenye mafanikio makubwa barani Afrika na duniani kote. Huku akivuma kimuziki, maisha yake ya kifamilia pia yamekuwa yakivutia mashabiki wengi, hasa kwa jinsi anavyohusiana na watoto wake.
Jada Pollock, anayejulikana pia kama Jada P, si tu mpenzi wa Wizkid bali pia ni meneja wake. Uhusiano wao wa kikazi na wa kimapenzi umeimarika kwa miaka, na sasa familia yao imekua zaidi. Kabla ya mtoto huyu wa tatu, wawili hao walikuwa tayari wamejaliwa watoto wawili, huku Wizkid akiwa na watoto wengine wawili kutoka mahusiano yake ya awali.
![](https://wasafimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/img_9836-1-628x1024.jpg)
Kwa sasa, bado hawajatoa maelezo zaidi kuhusu jina au jinsia ya mtoto wao Huyo. Hata hivyo, tukio hili limeongeza furaha katika familia ya staa huyo, huku akiwahakikishia mashabiki kuwa familia yake ni kipaumbele kikubwa kwake.
Hongera kwa Wizkid na Jada kwa zawadi hii ya maisha!
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.