Ayra Starr Ashambuliwa Na Mashabiki Baada Ya Kucheza Wimbo Wa Naira Marley

Muimbaji Wa Nigeria @ayrastarr Amejikuta Akishambuliwa Baada Ya Kucheza Ngoma Ya @nairamarley iitwayo “Pxy Drip”. Mashabiki wengi walionyesha kutoridhishwa na hatua hiyo, wakikumbusha kuhusu tuhuma zinazomkabili Naira Marley, hasa baada ya kifo cha Mohbad, ambaye alikuwa chini ya lebo ya Marley.

Mashabiki wanaamini kuwa Ayra Starr alipaswa kuonyesha msimamo na familia ya Mohbad na mashabiki wake kwa kuepuka kuunga Mkono kazi za Marley, ambaye bado anakabiliwa na lawama kutoka kwa Mashabiki.

Hata Hivyo #AyraStarr Baada Ya Kukosolewa Vikali Na Mashabiki Alichukua Hatua Ya Kuiondoa Video Hiyo Katika Mitandao Ya Kijamii

Video Ya Ayra Akicheza Ngoma Ya Naira Marley