Diamond Aahidi Kusaini Wasanii Wawili Kutoka Bongo Star Search Season 15

Mwanamuziki nyota wa Afrika, Diamond Platnumz, ameahidi kusaini wasanii wawili kutoka shindano la Bongo Star Search (BSS) Season 15 baada ya kuvutiwa na vipaji vilivyojitokeza kwenye fainali ya msimu huu.

Diamond, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Warehouse, Masaki, Dar es Salaam, alisema ameguswa na viwango vya washiriki na anaamini kuna nyota wapya wanaoweza kufika mbali kupitia lebo yake ya WCB Wasafi.

Katika fainali hiyo ya kusisimua, Moses Luka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo aliibuka mshindi wa kwanza, huku Saluh Kulwa kutoka Tanzania akishika nafasi ya pili, na Martha May kutoka Uganda akimaliza wa tatu.

Safari ya kuelekea fainali ilikuwa na ushindani mkubwa, ambapo katika Top 5, washiriki Prisca kutoka Babati na Grace kutoka Mwanza walionesha vipaji vya hali ya juu lakini walikosa nafasi ya kuingia hatua ya mwisho.