Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Tulia Ackson amewataka wanzania kuacha tabia ya kujidharau kwani Watanzania wanafanya vizuri katika Sekta mbalimbali za kiongozi Duniani
Dkt. Tulia ameyasema hayo Leo mei 19,2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akimpongeza Prof. Mohamed Janabi Kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani ukanda wa Afrika
Dkt. Tulia amesema kuwa nafasi hizo zinapatika sio Kwa bahati mbaya ila zinapatikana kutokana na mambo mazuri yanayofanyika ikiwa pamoja na utawala Bora
Ni jambo la kipekee Kwa Tanzania kupata Tena nafasi hiyo ikiwa Kwa mara ya kwanza nafasi hiyo ilishikiliwa na Marehemu Dkt. Faustine Ndungulile ambaye alifariki kabla ya kuanza majukumu yake
Leave a Reply