Msanii Wa Marekani Kevin McCall, ambaye aliandika Na Kushirikishwa na @chrisbrownofficial kwenye Wimbo Uitwao “Deuces” Wa 2010, Amejikuta akimwaga machozi Kwenye Podcast Ya @blackonfigg baada ya kuweka wazi kwamba kwa sasa anategemea msaada wa chakula cha serikali (EBT), ilhali ziara ya Chris Brown iitwayo “Breezy Bowl” imepata mafanikio makubwa kifedha
(Mapato) Ikiingiza Zaidi Ya Dola Milioni 90.

Kevin McCall Anasema Kuwa Anamdai Chris Brown Kiasi Cha $25K (Tsh Milioni 61.7/=) Kwa Nyimbo Nne (4) Alizomuandikia.
Hata Hivyo Baada Ya Post Hiyo Kusambaa Mtandaoni, Rapa Young Thug Aliibuka Na kusema Kuwa atamtumia Kevin McCall Kiasi Cha $25k (Tsh Milioni 61.7/=) na Kusema Kwamba anajua Chris Brown Atamsaidia.

Kumbuka Kevin McCall Alikuwa Chini Ya Label Ya Chris Brown ‘CBE’ na wamekwisha shirikiana kwenye nyimbo kama “Deuces,” “Strip,” na “No Bullshit”.

2016 Kevin McCall’ Aliibuka mtandaoni na kuomba kutolewa kwenye label ya Chris Brown baada ya kukosa maelewano ya kibiashara na boss wake. kevin Aliandika; “Nilijaribu kufanya biashara ya muziki kikubwa, lakini ukarimu wangu umefanya nidharaulike”. Kisha Breezy Akamjibu; “Endelea kubwabwajika Kevin, mimi ninaziweza hizo fujo za mtaani kuliko niwezavyo muziki. Endelea kuropoka uone utakavyofeli”.

Wawili Hawa waliendelea Kutupiana Vijembe, Ambapo Miaka 9 Iliyopita Chris Brown Alichia Video Akijigamba Kununua Nyumba Na Magari Ya Kifahari Kutokana Na Pesa Za Kevin McCall.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.