Kiungo wa Atlético Madrid, Antoine Griezmann ameomba msamaha kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na uamuzi wake wa zamani wa kujiunga na Barcelona, akieleza kuwa alikuwa kijana na hakuelewa thamani ya upendo aliokuwa akipewa na Atlético Madrid.
Nyota huyo wa Ufaransa amesema alitambua kosa lake baada ya kuondoka Atlético Madrid na baadaye kufanya kila alichoweza kurejea tena katika klabu hiyo ili kufurahia soka na mapenzi ya mashabiki hao.
“Naomba mnisamehe, nilikuwa kijana na nilifanya makosa kujiunga na Barcelona.
“Wakati huo sikuuelewa upendo niliokuwa nao hapa, Nilitambua kosa langu na nilifanya kila kitu kurejea tena na kufurahia kuwa hapa,” alisema Griezmann.
Griezmann pia amesema licha ya kutoshinda taji la La Liga wala UEFA Champions League akiwa Atlético Madrid, upendo kutoka kwa mashabiki ndiyo jambo lenye thamani kubwa kwake.
“Sikushinda La Liga wala UEFA Champions League, lakini upendo wenu ndiyo kitu muhimu zaidi,” alisema.





Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.