Baada ya kuchukua Carabao Cup, huko Newcastle ni kunywa kujigaragaza

Kufuatia ushindi wa Newcastle United wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool katika fainali ya Carabao Cup iliyochezwa jana, siku ya leo ni sherehe na mwendo wa kula nyama na bia huko Tyneside, England yaliko makazi ya mabingwa hao.

Newcastle ndio klabu pekee ya Ligi Kuu England ambayo nje ya uwanja wake wa St. James’s Park kuna vituo vingi zaidi vinavyouza pombe ambapo katika umbali wa maili moja kutoka uwanja huko kuna baa 174!

Hata mchambuzi wa soka England, Gary Neville alinukuliwa jana akisema kuwa siku ya leo hakuna shabiki wa Newcastle atakayeweza kwenda kazini kutokana na furaha waliyonayo ya kushinda kombe lao la kwanza tangu mwaka 1955.