Baba Mzazi amuua Mwanaye kwa Kipigo kisa hajarudisha Chenji Shilingi 9,000

Festo Isaya Nziku(39) Mkazi wa kitongoji cha Izyila Kata ya Mlowo Wilayani Mbozi Mkoani Songwe anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga maeneo mbalimbali ya mwili wake kwa fimbo, mateke na ngumi mwanaye Jackson Festo Nziku(10) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la Sita katika Shule ya Msingi Ivwanga iliyopo Wilayani humo tukio ambalo limetokea desemba 30 2024.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamshina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukiri kumshikilia baba mzazi ndugu Festo Nziku kwa tuhuma na kumpiga hadi kusababisha kifo cha mwanaye.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonesha ni kitendo cha marehemu Jackson kutorudisha chenji kiasi cha Shilingi elfu Tisa (9000) aliyopewa na baba yake ambaye ni mtuhumiwa baada ya kuagizwa kununua chapati.