Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku na Mahakama Kuu ya Tanzania kufanya shughuli zozote za kiutendaji mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa.
Kesi ya msingi, inayohusu mgawanyo wa rasilimali za chama hicho, imepangwa kuanza kusikilizwa Juni 24, 2025
Leave a Reply