Kevin De Bruyne ametangaza rasmi kwamba ataondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu wa 2024/25 baada ya kuhudumu kwa miaka kumi katika klabu hiyo.
Kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na City mwaka 2015 kutoka Wolfsburg kwa ada ya £55 milioni, na tangu wakati huo amecheza mechi 413, akifunga mabao 106 na kutoa pasi za mabao 174.
Katika kipindi chake na klabu ya Man City ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu, Kombe la FA mara mbili, na taji la Ligi ya Mabingwa.
Katika taarifa yake ya kuaga, De Bruyne alieleza shukrani zake kwa mashabiki, wachezaji wenzake, na jiji la Manchester kwa msaada wao katika safari yake ya soka. Alisema, “Jiji na klabu hii vimenipa kila kitu, na nimejaribu kutoa kila kitu kwao. Tumefanikiwa kushinda kila kitu pamoja.”
Kuhusu mustakabali wake, inaaminika kwamba De Bruyne anaelekea Major League Soccer (MLS) nchini Marekani, huku klabu ya San Diego FC ikiwa mstari wa mbele kumsajili. Hii inakuja licha ya klabu za Saudi Arabia pia kuonyesha nia ya kumsajili.

Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.