Kendrick Lamar ameweka historia kwa kutumbuiza kwenye onyesho la Halftime Show Ya Super Bowl LIX lililofanyika Februari 9, 2025, (Usiku Wa Kuamkia Leo) katika Uwanja wa Caesars Superdome, New Orleans. Akiwa msanii Kinara wa onyesho hilo, Lamar aliungana na wasanii wengine maarufu kama SZA, Samuel L. Jackson, Serena Williams, na Mustard.

Onyesho lilianza kwa Lamar na Dancers wake kushuka kutoka kwenye gari aina ya Buick Regal ya miaka ya 1980 na kupanda jukwaa lililofanana na kidhibiti cha mchezo wa PlayStation. Samuel L. Jackson alijitokeza kama Uncle Sam, Ndiye Aliyempandisha K-Dot Jukwaani. Mchezaji Wa tenisi Serena Williams alionekana Aki-Vibe wakati wa wimbo “Not Like Us”.
Wakati wa onyesho hilo, mtu mmoja alijaribu kuvuruga kwa kupeperusha bendera ya Palestina na Sudan, lakini alizuiwa haraka na maafisa wa usalama.

Kwa ujumla, onyesho la Lamar lilipokelewa vyema, likiwa na mchanganyiko wa nyimbo zake maarufu na ushirikiano na wasanii wengine, na hivyo kuacha alama isiyosahaulika katika historia ya Super Bowl.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.