Kijana DAZ Ajinyonga Kisa akiwa amevaa Gauni na Viatu vya Mpenzi wake

Kijana aliyefahamika kwa jina la Elirehema Ernest Mollel ‘DAZ’ (32) mkazi wa Kijiji cha Oldadai wilayani Arumeru Mkoani Arusha amekutwa amefariki kwa kujinyonga huku akiwa amevalia gauni na viatu vya kike ambavyo ni vya mpenzi wake.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa sababu ya kifo chake ni wivu wa kimapenzi, baada ya kuhitilafiana na mpenzi wake ambaye ni mwanachuo anayefahamika kwa jina la Bahati Gabriel na walikuwa wamefungua biashara Pamoja.

Baba Mzazi wa Marehemu, Ernest Mollel anasema anasema alipataa taarifa za kifo cha mwanaye leo asubuhi, na kuukuta mwili ukiwa umening’inia kwenye nyumba mbayo bado haijamalizika, huku akikata Kamba akidhani atamwokoa.

Ameongeza kuwa mwanaye alikuwa kijana mwenye kujituma, na hivi karibuni alimshauri yeye na mpenzi wake wafunge ndoa.

Lomayani Kivuyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldadai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku polisi wakifika eneo hilo kuchukua mwili wa marehemu.