Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Mhe. Hamisi Shaban Taletale, maarufu kama Babu Tale, amepongeza juhudi kubwa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kutekeleza ahadi za maendeleo kwa wananchi.
Kupitia ujumbe wake aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Mhe. Babu Tale amesema, “Kila tambo ina sababu, na haiwezi kuwa sababu ya hovyo bali sababu yenye mafanikio. Hapa natamba kwakuwa kila tulichowaahidi kinatekelezwa kwa kasi kubwa. Asante Mh Rais Samia_Suluhu_Hassan.”

Mbunge huyo aliendelea kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na kumuunga mkono Rais Samia katika juhudi zake za kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka na yenye tija. Katika hatua ya kuhamasisha mshikamano, aliongeza kwa kusema:
“Hivi vitambo sababu kubwa ni wewe Mama. Sasa naomba tuimbe pamoja jamani…. MWAMBIENI, MWAMBIEENI…”
Ujumbe huo umeibua shangwe miongoni mwa wananchi wa jimbo hilo ambao wanaona juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha maisha ya wananchi. Babu Tale ni miongoni mwa viongozi wa Bunge wanaoonyesha mshikamano wa karibu na Serikali kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya taifa.

Leave a Reply