Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa akikipiga kunako ligi kuu ya nchini Zambia, Eliuter Mpepo yupo mbioni kusaini mkataba mpya kujiunga na nyuki wa Tabora (Tabora United) ambapo tayari wawili hao wamesaini mkataba wa awali.
Aidha mchezaji huyo amegeuka Lulu kwenye Ligi Kuu ya NBC baada vilabu vingine kuingilia dili hilo wakiitaka saini ya Mshambuliaji huyo nyota aliyewahi kukipiga Mtibwa Sugar, Tz Prisons, Singida Utd, Build Con na Trident zote za Zambia na Interclube ya Angola.
Waajiri wake wa zamani, Tz Prisons wao wameenda mbali zaidi na tayari wapo kwenye mazungumzo na nyota huyo ili kuweza kuinasa saini ya Mshambuliaji huyo aliyewahi kufanya makubwa akiwa nao hapo awali.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.