Mzee wa Miaka 73 ajinyonga kisa Msongo wa Mawazo Shinyanga.

Kufuatia tukio lililotokea hapo jana Januari 06, 2025 majira ya saa kumi za jioni katika mtaa wa Azimio Kata ya Lubaga ndani ya manispaa ya Shinyanga la kujinyonga kwa mzee aliyefahamika kwa jina la Joseph Tuju (73) mkazi wa mtaa wa Azimio huku chanzo kikiwa hakijafahamika, Mwandishi watu kutoka mkoani humo Abel Michael amezungumza na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga SACP. Janeth Magomi kupata ufafanuzi wa tukio hilo

SACP. Janeth Magomi amesema Joseph Tuju alijinyonga kwa kutumia shuka ndani ya nyumba yake, chanzo kikiwa ni msongo wa mawazo kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbu ndipo alichukuwa uamuzi wa kujinyonga.

Aidha kamanda Magomi ametoa rai kwa watu kutojichukulia sheria mkononi na kupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali kwenye maisha.