Rapa Nicki Minaj ameuzua taharuki mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe unaoonyesha wazi kukerwa kwake na Jay-Z, kiasi cha kuamua kusitisha mipango ya kutoa albamu yake mpya.

Katika tweet hiyo iliyosambaa sana, Malkia Nicki Minaj aliandika:
“Sawa sitatoa tena album. Hakuna muziki zaidi. Natumai unafurahi sasa sc. Kwaheri, Barbz. Nawa penda maisha yote.”
Kutajwa kwa handle sc, ambayo ni kifupi cha Shawn Carter (jina halisi la Jay-Z), kunathibitisha kuwa ujumbe huo ulimlenga moja kwa moja. Hatua hii imekuja huku kukiwa na historia ya mvutano kati ya Nicki Minaj na Jay-Z, hasa ikihusisha masuala ya kibiashara na kampuni yake ya Roc Nation.
Uamuzi huu wa kusitisha muziki wake umeacha mashabiki wake, wanaojulikana kama Barbz, katika sintofahamu kubwa huku wengi wakishuku kuwa huenda kitendo hicho ni dhihirisho la hasira ya muda mfupi au ni mbinu ya kuteka hisia.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.