Kocha wa Manchester United, Ruben Amorim, amesisitiza kuwa hatajiuzulu kutoka klabuni licha ya msimu mbaya wa timu hiyo. Amorim amesema yuko tayari kuondoka bila kudai fidia yoyote endapo bodi ya klabu au mashabiki wataona kuwa hafai kuendelea na kazi hiyo.
Kauli hii imekuja baada ya Manchester United kupoteza fainali ya Europa League kwa kufungwa 1-0 na Tottenham Hotspur, matokeo ambayo yameifanya timu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao. Kwa sasa, United inashikilia nafasi ya 16 katika Ligi Kuu ya England, ikiwa na ushindi 16 tu kati ya mechi 41 tangu Amorim achukue nafasi ya ukocha mwezi Novemba mwaka jana.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Amorim alisema:
‘Kama bodi na mashabiki wataona mimi sifai kuwa kocha, nitaondoka siku inayofuata bila kudai fidia yoyote… lakini sitaacha kazi kwa hiari. Nina imani kubwa na kazi ninayofanya, hata leo.’
‘Kama mnavyoona, sita badilisha chochote katika namna ninavyofanya mambo. Mnajua kuwa huwa niko wazi na mkweli kila wakati…’”
Amorim pia alikiri kuwa kuna changamoto kubwa ndani ya klabu na kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika katika kipindi cha majira ya joto. Alisisitiza kuwa anahitaji muda na imani kutoka kwa mashabiki ili kuleta mabadiliko chanya.
Licha ya kuwa na mkataba hadi mwaka 2027, Amorim amekiri kuwa nafasi yake ya kazi iko hatarini kutokana na matokeo mabaya ya timu. Hata hivyo, anasisitiza kuwa anaendelea kujitahidi kurekebisha hali hiyo na kuifanya Manchester United kuwa timu ya ushindani tena.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.