Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo Mei 19, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:
Prof. Tumaini Nagu: Ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia masuala ya afya.
Dkt. Blandina Kilama: Amteuliwa kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu. Dkt. Kilama anachukua nafasi ya Dkt. Lorah Madete ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa majukumu mengine.
Balozi George Kahema Madafa: Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania. Anachukua nafasi ya Dkt. Majige Budeba ambaye amemaliza muda wake.
Bw. Jacob Jail Kibona: Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kipindi cha pili.
Meja Jenerali Mstaafu John Julius Mbungo: Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) kwa kipindi cha pili.
Bw. Mussa Hamza Mandia: Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kipindi cha pili.
Leave a Reply