Rio achukizwa na kauli ya Amorim juu ya Rashford

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini, Marcus Rashford (27) hana mustakabali tena katika klabu hiyo baada ya meneja, Ruben Amorim kusema afadhali kuwa na kocha wake wa makipa katika kikosi chake kuliko kuwa na Rashford.

Rashford hajaichezea United tangu Desemba 12, huku Amorim akimuacha nje ya kikosi kwa kila mechi kando na mchezo mmoja, ambao alikuwa akitokea benchi na hakutumika.

Alipoulizwa kwa nini hakumjumuisha Rashford katika mechi ya Jumapili ya 1-0 dhidi ya Fulham, Amorim alijibu ni bora kumchezesha Kocha wa Makipa Jorge Vital, mwenye umri wa miaka 63.

“Sote tuna siku za mbaya au wakati ambapo hatufanyi vizuri, tunakosa kujiamini, lakini bidii sio moja ya mambo ambayo ningetaka kusikia kutoka kwa meneja akisema kuwa ni chanzo cha mimi kupungukiwa.

“Hayo ni maoni ya kuchukiza, kwa sababu nadhani anajua majibu ni nini baada ya maoni hayo.

Hasemi hivyo bila kufikiria, ‘Hii inaelekea wapi?’ Kwa kweli hakuna njia ya kurudi kwa Marcus baada ya hapo, sidhani, na aina hiyo ya maoni kutoka kwa Kocha wake.” Amesema Rio.