Simba yafuzu robo fainali Shirikisho Afrika

Baada ya Simba Sc kupata sare ya mabao 1-1 dhidi ya Bravos ya Angola ni rasmi kuwa wametinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa wamefikisha Jumla ya alama 10 nyuma ya CS Constantine wenye alama 12. 

Simba wamebakiza mchezo mmoja wa mwisho dhidi ya CS Constantine katika hatua hii ya Makundi ambapo watakuwa wakipambania kuongoza kundi hilo.

Bravos wenye alama 7 hawatakuwa na uwezo wa kufuzu hatua inayofuta hata wakipata ushindi dhidi ya CS Sfaxien kutoka na kanuni ya (Head to Head) ambapo Simba alishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Bravos na sare katika mchezo wa pili hivyo anafanikiwa kuwa mbele ya Bravos hata wakipa ushindi wowote na Simba kupoteza mchezo dhidi ya Constantine.