Taasisi Ya Beyonce “BeyGood” Yachangia Zaidi Ya Tsh Bilioni 6.3 Janga La Moto California

Beyonce Kupitia Taasisi Yake, Iitwayo “BeyGood”,  Ameripotiwa Kuchangia Kiasi Cha $2.5m (Tsh Bilioni 6.3/=) Ili kusaidia Walioathirika na moto mkubwa unaoendelea huko Los Angeles.

BeyGood, Imelenga kuwapa wahanga misaada ya dharura, kama vile chakula, malazi, na huduma za afya ya akili, huku pia ikisaidia miradi ya ujenzi N.k. Hatua hii ni mfano wa jinsi mastaa na mashirika yao wanavyoweza kutumia ushawishi wao kusaidia watu walioko kwenye hali ngumu.

Beyoncé amekuwa akisisitiza umuhimu wa kusaidia jamii zilizo na uhitaji mkubwa kupitia Mashirika na kampeni mbalimbali, na mchango huu unadhihirisha dhamira yake ya kusaidia wale walioko katika wakati mgumu.