Viongozi, wananchi wapongeza uzinduzi wa jengo la halmashauri Bumbuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Januari 24, 2025 ameweka jiwe la ufunguzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli lenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.5.

Baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo hilo, Rais Dkt. Samia alipata wasaa wakuzungumza na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Lushoto.

Aidha wananachi hao wa lushoto wamempongeza Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu kama maji, elimu, afya na barabara.

Rais Samia yuko Mkoani Tanga kwenye ziara ya kikazi ya siku saba iliyoanza jana Januari 23 na anatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.