Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambaye ni mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mapinduzi imekubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wao wa raundi ya pili waliocheza dhidi ya Burkina Faso 🇧🇫 katika michuano hiyo.
Burkina Faso wanajikusanyia jumla ya Alama nne baada ya kupata sare katika mchezo wa kwanza dhidi ya Kenya, na ushindi dhidi ya Zanzibar Heroes huku Zanzibar wao wakibakiwa na alama tatu walizovuna mbele ya Kilimanjaro Stars katika mchezo wao wa raundi ya kwanza.
Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba, kuanzia saa 1:00 usiku.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.